mpenzi wangu amepoteza usichana wake baada ya kubakwa

Question

Nina mpenzi wangu wote tunasoma a level ana miaka 19, tuna date sasa mwaka wa 3 tulikubaliana tusisex had tutakapokuwa tayari, tunapendana na tuna mipango mingi future. Jana wakati tuna chat alinambia kuwa mwezi wa 12 alipokuwa likizo alibakwa na mpangaji anayekaa nyumba moja na Dada yake na kumsababishia apoteze usichana wake. Mwanzoni nilipaniki nikidhan labda alinicheat ila baada ya kunambia vizuri ninamuonea huruma sana kwa sababu Nina muamini yeye ni mcha mungu sana na alikuwa anatunza usichana wake sababu ana hofu ya mungu na hakupenda kumpa zawad ya usichana wake MTU ambaye amembaka. Bahati mbaya hakureport hilo tukio kokote Jana ndio akaamua aniambie mm ukweli. Nimejaribu kumbembeleza asahau yote nimeshindwa na ninaumia kwa kuwa ni MTU ninayempenda sana na mwezi wa 5 anatakiwa afanye mtihan wa form six. Please naombeni ushauri nimsaidie VP kwa kuwa hata familia yake haijui chochote ameamua kuniambia Mimi ili angalau moyo Wake utulie bado nampenda sana na nipo tayari kuendelea na nae naomba mnisaidie

Anonymous 2 years 4 Answers 189 views 0

Answers ( 4 )

 1. Jambo la kwanza jaribu kumwondoa hofu mwathiriwa na
  muliwaze maana amepata jambo la kutisha. Na iwapo mtu
  amejeruhiwa sana mpeleke katika kituo cha huduma za afya
  kilicho karibu mara moja.!

 2. Usimweleze kila mtu kilichotokea. Waeleze wale tu
  ambao unafikiri wanaweza kusaidia kama daktari, mwalimu au
  mzazi. Usiulize maswali ya kwa nini maana inaweza ikaonekana
  ni kosa la mwathiriwa. Badala yake zungumza na huyo mtu kwa
  utaratibu, polepole, peke yake na mpe uangalifu wa kutosha.
  Hakikisha kwamba hutoi lawama yoyote kwa mwathiriwa.
  Kubakwa kamwe siyo kosa la mwathiriwa.

 3. Allah razı olsun kardeşim

 4. chakwanza mshauri akapime ukimwi na mimba ili ajue afya yake ikoje maana uwezi jua yule aliye mbaka yuko salama au laa, Jaribu kumshauri atoe taarifa kwa walezi wake au hata kwenye vyombo vya usalama na wewe Jaribu kuwa nae Jaribu sana ili kumpa moyo kwenye kipindi hiki kigumu ujita hidi ili asijisikie yuko mpweke.

Leave an answer

Sorry, you do not have a permission to answer to this question .